Kumb : TANESCO SACCOS / MKUTANO MKUU/2022 Tarehe 01/10/2022
Wawakilishi wote, Mkutano Mkuu wa Mwaka, TANESCO SACCOS LTD.
YAH: TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA MWAKA 2022
Bodi ya Chama inawatangazia wanachama wote wawakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama, kwamba Mkutano Mkuu wa Mwaka 2022 utafanyika Dar es salaam tarehe 22 na 23 Oktoba 2022 katika ukumbi wa Mikutano wa APC- Hotel and Conference Centre, Uliopo Bunju jijini Dar es salaam kuanzia saa 02.00 asubuhi.
AJENDA:
1. Kufungua Mkutano
2. Muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2021
3. Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa mwaka 2021
4. Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chama
5. Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2021
6. Taarifa ya Kamati ya Usimamizi
7. Mpango kazi na Bajeti ya mwaka 2023
8. Kuidhinisha Wakaguzi wa hesabu za mwaka 2022
9. Mengineyo
10. Kufunga Mkutano
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
1. Mengineyo yatumwe Makao Makuu ya Chama kabla ya tarehe 05/10/2022
2. Wawakilishi wote watajisajili katika Ukumbi wa APC Hotel and Conference Centre, Bunju siku moja kabla ya Mkutano (Tarehe 21.10.2022)
3. Wawakilishi wote wanatakiwa kuja na vitambulisho vyao vya kazi.
4. Mwisho wa kusajili wajumbe wa Mkutano Mkuu ni saa 02.00 kamili asubuhi.
5. Nakala chepe ya kabrasha la Mkutano Mkuu litatumwa Matawini kwa njia ya mtandao tarehe 15.10.2022. Nakala halisi za kabrasha zitatolewa katika viunga vya APC Hotel and Conference Centre, Bunju siku moja kabla ya Mkutano.
Pamoja na salaam za Ushirika.
Somoe I. Nguhwe.
MWENYEKITI
Nakala:
• Afisa Ushirika, Manispaa ya Ubungo, Dar es salaam
• Mrajis Msaidizi wa Mkoa, Dar es salaam
• Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Dodoma.
• Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu, TANESCO – Makao Makuu