TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA MWAKA 2023

Kumb: TANESCO SACCOS / MKUTANO MKUU/2023  Tarehe: 01/11/2023

Wawakilishi wote, Mkutano Mkuu wa Mwaka, TANESCO SACCOS LTD.

YAH: TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA MWAKA 2023

Bodi ya Chama inawatangazia wanachama wote wawakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama, kwamba Mkutano Mkuu wa Mwaka 2023 utafanyika Dar es salaam tarehe 25 Novemba 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, uliopo jijini Dar es salaam kuanzia saa 02.00 asubuhi.

AJENDA:
1. Kufungua Mkutano
2. Muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2022
3. Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa mwaka 2022
4. Taarifa ya Bodi ya Chama
5. Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2022
6. Taarifa ya Kamati ya Usimamizi
7. Mpango kazi na Bajeti ya mwaka 2024
8. Kuidhinisha Wakaguzi wa hesabu za mwaka 2023
9. Uchaguzi – Wajumbe wa Bodi na K/Usimamizi
10. Mengineyo
11. Kufunga Mkutano

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
1. Mengineyo yatumwe Makao Makuu ya Chama kabla ya tarehe 15/11/2023
2. Wawakilishi wote watajisajili katika ofisi za Chama zilizopo Shekilango siku moja kabla ya Mkutano (Tarehe 24.11.2023)
3. Wawakilishi wote wanatakiwa kuja na vitambulisho vyao vya kazi.
4. Mwisho wa kusajili wajumbe wa Mkutano Mkuu ni saa 02.00 kamili asubuhi.
5. Nakala chepe ya kabrasha la Mkutano Mkuu litatumwa Matawini kwa njia ya mtandao tarehe 18.11.2023. Nakala halisi na link ya taarifa mbalimbali za Mkutano itatolewa katika viunga vya Ukumbi wa Mlimani City siku ya Mkutano na Ofisini wakati wa Usajili.

Pamoja na salaam za Ushirika.

Download

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *