TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA BODI NA KAMATI YA USIMAMIZI

Kumb Na: TANESCO SACCOS/UCHAGUZI/2023 Tar: 02 Nov 2023

WAWAKILISHI, TANESCO SACCOS

YAH : UCHAGUZI WA VIONGOZI WA BODI NA KAMATI YA USIMAMIZI

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo TANESCO kinapenda kuwatangazia wawakilishi wote kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Novemba 2023, Katika Mkutano Mkuu wa mwaka 2023

Zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa fomu litaanza tarehe 02 Novemba 2023 hadi tarehe 16 Novemba 2023.

Fomu za Uchaguzi zinapatikana ofisi za Chama Shekilango na kwenye tovuti ya Chama, mfumo wa urejeshwaji wa fomu zitapokelewa:

• Kupitia Ofisi za Chama au njia ya barua pepe info.saccos@tanescosaccos.or.tz
Kwa kuzingatia masharti ya Chama, vigezo vya uongozi ni pamoja na vile vilivyobainishwa katika sehemu ya 10, kifungu namba 55(b) cha Masharti ya Chama (Tafadhali pakua masharti ya Chama katika tovuti ya Chama na kuyapitia). Hakikisha unaambatanisha nakala ya cheti cha kuhitimu Chuo (Stashahada ya juu/Shahada.)

Maelezo na Maulizo Zaidi piga namba za ofisi 0737584782 au 0733140107

Andrea Hilary
Meneja

Download

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *