Chama kinawatangazia Wanachama wote kuwa, kinatarajia kuanza kufanya Mikutano ya Mrejesho wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2023 katika matawi yake nchi nzima kuanzia tarehe 16.03.2024 ili kuwajulisha juu ya maamuzi yaliyofikiwa na kuwapatia taarifa mbalimbali za maendeleo ya Chama. Agenda za Mkutano:
- Taarifa : Dondoo na Majibu
- Hesabu za Chama kuishia Disemba 2022
- Maazimio ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2023
- Mwanachama Mzalendo (Member loyalty)
- Uchaguzi wa Wawakilishi – Matawini
- Usajili wa Wanachama katika mfumo wa FOSA mobile – USSD
NB:
- Mwanachama atajisajili katika rejesta ya mahudhurio na rejesta hiyo itafungwa na Mwenyekiti wa Mkutano dakika 45 baada ya Mkutano
- Bajeti ya maandalizi itumwe kwa Meneja wa Chama na Posho italipwa kwa wanachama waliohudhuria kikao tu (sitting allowance).
- Ukumbi wa semina lazima uwe na mazingira ya kufanya wasilisho (Presentation- Softcopy), hatutakuwa na vipeperushi. Pia zingatia uwepo wa Kangavuke (Generator).
Download Presentation Guide here