BOSA

Activity (BOSA) Products and Services.

 

 1. 1
  Mkopo wa Maendeleo (Development loan)

  Mkopo huu utatokana na Akiba na hisa za wanachama,na mkopo huu utakopeshwa kwa madhumuni ya ujenzi,ufugaji, upanuzi wa mashamba pamoja na ununuzi wa vyombo vya usafiri.

  • Mwanachama ana uhuru wa kukopa kiwango ambacho hakizidi mara Tatu (4) ya akiba alizonazo katika Chama
  • Kiwango cha juu cha mkopo kitakuwa Tshs. 100,000,000.00 Hii itategemea zaidi uwezo wa mshahara wa mwanachama husika
  • Muda wa marejesho ya mkopo ni hadi miezi arobaini na nane (60) kulingana na matakwa ya mwanachama mwenyewe
  • Mwanachama ataruhusiwa kukopa tena iwapo atakuwa amemaliza mkopo wa awali, au amerejesha theluthi moja (1/3) ya deni la awali
  • Mwanachama ataruhusiwa kutunisha akiba zake kwa kuingiza fedha taslim katika akaunti ya Chama na atakuwa na haki ya kukopeshwa kutokana na akiba yake hiyo miezi mitatu baada ya kutunisha akiba yake
  • Riba kwa mkopo wa maendeleo ni asilimia 1.2% kwa mwezi kwa baki ya mkopo (Reducing Balance Method)
  • Mkopo huu una kinga ya Bima ambayo italipwa na mkopaji.
  • Mkopo huu hautatolewa iwapo baki ya mshahara wa mwanachama itakuwa chini ya theluthi moja (1/3)
  • Mwanachama atakayekopa Mkopo na kulipa kupitia pensheni ya mwezi atakopa mkopo huu asilimia 100 ya akiba zake.Muda wa marejesho na riba zitakuwa kama zilivyoanishwa katika kipengere(c) na (f).Mkopo wa kwanza hautakuwa na wadhamini.Mkopo wa pili(mara mbili ya akiba na hisa za hisa za hiari) utakuwa na wadhamini na dhamana nyinginezo kama taratibu kama zilinyoainishwa katika kifungu namba 1.8.
 2. 2
  Mkopo wa Dharura (Emergency Loans)
  • Mkopo huu utatolewa kwa wanachama kwa kiwango cha kuanzia Tshs.300, 000.00 hadi Tshs.3,000,000.00 na itategemea zaidi uwezo wa mshahara wa mwanachama na akiba alizonazo katika Chama.
  • Mkopo wa dharura hautatolewa kwa mwanachama ambae atakuwa bado hajamaliza mkopo wa awali (Dharura).
  • Makato kwa mkopo ya dharura yatafanyika kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili.
  • Riba kwa mikopo ya dharura itakuwa asilimia 2 kwa mwezi kwa baki ya mkopo.
 3. 3
  Mkopo wa Elimu (Education Loans)
  • Kiwango cha mkopo wa Elimu ni mshahara hakitazidi mara mbili ya mshahara wa mwanachama.
  • Riba ya mkopo wa Elimu ni asilimia tano (5%) ya kiwango cha mkopo.
  • Makato kwa mkopo wa Elimu yatafanyika kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na miwili.
  • Mwanachama atalazimika kuwa na barua ya madai ya shule ambayo anatarajia kulipa ada yake mwenyewe, mtoto au mtegemezi wake.
  • Mwanachama atakayekopa mkopo na kulipa kupitia pensheni ya mwezi atakopa mkopo huu mara moja au mbili ya pensheni  ya mwezi  kuulipa ndani ya kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili.
  • Mkopo wa Elimu hautatolewa kwa mwanachama ambae atakuwa bado hajamaliza mkopo wa pili.
 4. 4
  Mkopo wa Papo kwa Papo (Salary Advance)
  • Utatolewa kwa kiwango cha kuanzia Tshs50, 000 hadi Tshs.150,000.00 kuanzia tarehe 10 hadi 20 ya kila mwezi unaofuata.
  • Makato ya marejesho ya mkopo huu yatafanyika mwezi unaofuata. kwa mkupuo mmoja.
  • Riba ya mkopo wa papo kwa hapo ni asilimia 10%. tu.

  Tanbihi: Mwanachama wa kundi la waajiriwa wa muda(temporary employees) atanufaika na bidhaa zote za chama na atapaswa kulipa mkopo huo ndani ya muda wa mkataba uliosalia.