FOSA

Mikopo yote ya FOSA itatolewa kwa wanachama ambao mishahara yao inapitia kwenye account zao za FOSA

 

 1. 1
  Mkopo wa Boresha Maisha
  • Mwanachama  anauhuru wakukopa kiwango ambacho hakizidi maratano(5) yamshahara wake wa mwezi.
  • Riba ya mkopo huu itakuwa asilimia 1.2 kwa mwezi kwa baki ya mkopo.
  • Muda wa juu wa marejesho ya mkopo nimiezi(60).
  • Mwanachama ataruhusiwa kukopa tena iwapo atakuwa amemaliza mkopo wa awali,au amerejesha nusu(1/2) ya marejesho yadeni la wali.
  • Mwajiri/Mfuko wa hifadhi ya jamii utakuwa mdhamini wa mkopo huu kwakuhakikisha mshahara/pensheni wa mfanyakazi unapita katika akaunti ya mwanachama ndani ya chama.Lakini pia mwanachama anaweza kufanya marejesho kupitia standing order.
 2. 2
  Mkopo wa Chipukizi
  • Mkopo huu utatolewa kwamwanachama ambaye ameajiriwa ndani  ya kipindi cha miezi kumi na mbilina awe amethibitishwa kazini.
  • Mwanachama anaweza kukopa kiwango ambacho hakizidi maratano(5) yamshahara wake wamwezi.
  • Riba  yamkopo huu itakuwa asilimia 1.3 kwa mwezi kwabaki yamkopo(Reducing Balance Method).
  • Muda wa juu wa marejesho ya mkopo ni Miezi kumi na mbili (12) kwa mwanachama mwenye mkataba wa muda mfupi na miezi ishirini na nne(24)kwa mwenye mkataba wa muda mrefu.
  • Mwajiri atahakikisha mshahara wa mfanyakazi unapita katika akaunti ya mwanachama ndani ya Chama.
 3. 3
  Mkopo wa Matangulizi ya Mshahara
  • Mwanachama anaweza kukopa kiwango kuanzia asilimia 10hadi 25 ya mshahara wa mwezi.
  • Riba ya mkopo huu itakuwa asilimia 10 kwa mwezi kiasi cha mkopo.
  • Mkopo huu utarejeshwa mwezi unaofuata.
  • Mwajiri atakuwa mdhamini wa mkopo huukwa kuhakikisha mshahara wa mfanyakazi unapita katka akaunti ya mwanachama ndani ya Chama.
 4. 4
  Mkopo wa Ujasiriamali
   • Riba ya mkopo huu itakuwa asilimia 3.75kwa mwezi
   • Muda wa juu wa marejesho ya mkopo ni miezi ishirini na nne(24).
   • Dhamana za mkopo huu  zitakazo kubalika nipamoja na hati ya nyumba, kiwanja, hati ya shamba,au kadi hali siya gari.
   • Pamoja na masharti  ya kipengele(d) mwanachama atatakiwa kuwasilisha :Leseni yabiashara,namba ya utambulisho wa mlipakodi na mpango wa biashara.
   • Mwanachama atatathimiwa kwa kigezo cha kufanya miamala katika akaunti yake ndani ya Chama angalau mara tatu kwamwezi.
   • Marejesho ya mkopo huu yataanza  baada ya miezi (3).

   Tanbihi: Mwanachama wa kundi la waajiriwa wa muda(temporary employees)atanufaika na bidhaa zote za Chama na atapaswa kulipa mkopo huo ndani ya muda wamkataba uliosalia.

 5. 5
  Mkopo Wa Gari
  • Mwanachama atahitaji kuchagua gari ambalo atataka chama kilinunue katika website ya beforward au SBT.
  • Mwanachama anaweza kukopa kiwango cha juu cha gari ambacho ni Tshs 50,000,000/=
  • Riba  yamkopo huu itakuwa asilimia 0.8 kwamwezi.
  • Muda wa juu wa marejesho ya mkopo ni Miezi thelathini na sita (36)
  • Mwajiri atahakikisha mshahara wa mfanyakazi unapita katika akaunti ya mwanachama ndani  ya Chama.

  Marejesho ya mkopo huu yataanza  baada ya mwanachama kupokea gari lake

 6. 6
  Mkopo Wa Wekeza
  • Mwanachama anaweza kukopa kiwango ambacho hakizidi mara mbili (2) ya hisa zake za hiari.
  • Riba  yamkopo huu itakuwa asilimia 8 kwa mwezi
  • Muda wa juu wa marejesho ya mkopo ni Miezi kumi na mbili (12).

  Mwajiri atahakikisha mshahara wamfanyakazi unapita katika akaunti ya mwanachama ndani ya Chama