Q

Ni nani awezaye kujiunga Tanesco Saccos? Na ili ajiunge anapaswa kuwa na Vigezo gani?

A

Uanachama ndani ya TANESCO SACCOS uko wazi kwa Mwajiriwa/mstaafu wa Shirika la Umeme TANESCO, TANESCO SACCOS, Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake, na Kampuni nyinginezo zitakazokubaliwa na Bodi ya Chama.

Q

Nitawezaje kujiunga na Tanesco Saccos Mobile Banking?

A

Mwanachama anaweza kujisajili kwa kupakua App ya Tanesco saccos kwenye Playstore kupitia simu yake ya mkononi, kisha atapokea OTP ambayo itamuwezesha kubadili PIN/password anayoitaka.

Q

ATM Card yangu naweza kuitumia wapi, au kwenye Benki zipi naweza kupata huduma?

A

Unaweza kutumia kadi yako ya FOSA kwa Wakala wa TCB/TPB , ATM za TPB/TCB, Pamoja na ATM zote za UMOJA SWITCH.

Q

Ni hatua zipi za kufuata ikiwa Mwanachama anataka kujitoa chama?

A

Mwanachama anatakiwa kuandika Barua kwa Mwenyekiti wa chama kuelezea nia yake ya kujitoa chama pia Mwanachama anatakiwa aweke namba ya Account ya Bank ambayo itatumika kufanya Malipo, namba za simu kwa ajili ya mawasiliano na Malipo ya Kujitoa yatafanyika siku 60 toka tarehe ya maombi hayo kuwasilishwa ofisini.

    Uliza swali lako