Mkopo wa Elimu

  1. Kiwango cha mkopo wa Elimu mwanachama anaweza kukopa kiwango cha mishahara yake miwili..
  2. Riba ya mkopo wa Elimu ni asilimia tano (5%) ya kiwango cha mkopo.
  3. Makato kwa mkopo wa Elimu utafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu (3) mpaka miezi kumi na miwili (12) kulingana na matakwa ya mteja.Kiwango cha akiba alizonazo kitazingatiwa.
  4. Mkopo wa Elimu hautatolewa kwa mwanachama ambae atakuwa bado hajamaliza mkopo wa awali (Elimu).
  5. Mwanachama atalazimika kuwa na barua ya madai ya shule ambayo anatarajia kulipa ada yake mwenyewe, mtoto au mtegemezi wake.