Taratibu za Kujiunga

  1. Mfanyakazi anayetaka kuwa Mwanachama atapeleka maombi kwenye Bodi ya Chama kwa kujaza fomu maalum ya maombi iliyobandikwa picha ya mwombaji.
  2. Ndani ya kipindi cha siku tisini (90) Bodi iwe imeshughulikia ombi/maombi na kutoa jibu la kukubali au kukataa kwa mwombaji/waombaji kuwa Mwanachama.
  3. Mwombaji akikubaliwa kujiunga na chama atalipa kiingilio cha TShs. 10,000.00 na kununua hisa zisizo pungua mbili (2) zenye thamani iliyoonyeshwa katika sehemu ya nne (4) ya masharti haya kati ya hisa ishirini (20) za mwanzo anazotakiwa kununua kwa mujibu wa Masharti haya.
  4. Sehemu ya hisa zilizobaki ni lazima zilipwe katika kipindi kisichozidi miezi tisa (9) tangu kujiunga kwake. Aidha Mwanachama ataendelea kuchangia akiba zake kila mwezi (mafungu) kwa kiasi kisichopungua TShs. 30,000.00 au kiasi ambacho kitakuwa kimepangwa na wanachama kulingana na wakati.
  5. Chama kitakuwa na Daftari la Wanachama lenye maelezo muhimu ya Mwanachama yakihusisha hisa, kiingilio, mafungu yake ya kila mwezi na majina ya warithi, kwa kuandikwa wazi, na kila Mwanachama atatia saini/dole gumba la kulia mbele ya jina lake.