Wajibu wa Mwanachama

Kila mwanachama wa Ushirika huu atawajibika kwa Chama kama ifuatavyo:-

  1. Kulipa kiingilio, kununua hisa na kulipa akiba ya kila mwezi kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizowekwa. Aidha anatakiwa atoe michango yote anayotakiwa kutoa kama itakavyoamuliwa katika Mkutano Mkuu.
  2. Kulipa madeni yote katika chama kwa ukamilifu na kwa wakati unaokubalika.
  3. Kubeba (Liability) dhima iwapo janga lolote litatokea. Dhima hiyo kikomo chake ni kiasi cha hisa zake katika Chama.
  4. Kuhudhuria vikao vya Chama tawini kila vinapoitishwa na kushiriki kikamilifu katika vikao hivyo na kutekeleza maamuzi ya Mkutano Mkuu.
  5. Kuheshimu mikataba ikiwa ni pamoja na kulipa mkopo alioudhamini endapo mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake kama alivyoahidi bila sababu za msingi.
  6. Kununua hisa pamoja na kuchangia akiba kwa mujibu wa masharti haya, kifungu Na. 5 c. na d.
  7. Kuyaelewa masharti ya Chama na kuyafuata pamoja na kuzielewa na kuzifuata sheria na kanuni za vyama vya ushirika, nyaraka za Mrajis wa vyama vya Ushirika na sera za chama.
  8. Kudhamini na kutetea Chama pamoja na Wanachama wake pale ambapo hali ambayo haitoi sura nzuri inapojitokeza, kupitia kamati ya usimamizi, Bodi, au kwa mwakilishi wa wanachama kwa maandishi au Mrajis wa vyama vya Ushirika.