• Mkutano Mkuu wa TANESCO SACCOS 2020
  Wajumbe wastaafu wa bodi ya chama cha ushirika Tanesco Saccos
 • Mkutano Mkuu wa TANESCO SACCOS 2020
  Mrajis wa vyama vya ushirika na mtendaji mkuu wa tume ya maendeleo ya ushirika tanzania Dkt. Benson Ndiege kwenye picha ya pamoja na wajumbe wastaafu wa bodi ya chama cha ushirika Tanesco Saccos.
 • Mkutano Mkuu wa TANESCO SACCOS 2020
  Monica Massawe mshindi wa tuzo wa mtumiaji bora wa bidhaa za Fosa kwa mwaka 2020.
 • Mkutano Mkuu wa TANESCO SACCOS 2020
 • Mkutano Mkuu wa TANESCO SACCOS 2020
  Wajumbe/ wawakilishi wa matawi kwa mkutano mkuu wa mwaka 2020
 • Mrajis wa vyama vya ushirika na mtendaji mkuu wa tume ya maendeleo ya ushirika tanzania Dkt. Benson Ndiege akikabidhi tuzo kwa washindi wa bidhaa mbalimbali za Tanesco Saccos mkutano mkuu kwa mwaka 2020.

Karibu TANESCO SACCOS

TANESCO SACCOS ni Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Shirika la Umeme – TANESCO ambao wamejiunga pamoja kwa hiari kwa madhumuni ya kuinua na kustawisha hali ya uchumi na maisha yao kwa kuanzisha na kumiliki TANESCO SACCOS kidemokrasia, kuchangia mtaji na kukubali kuyakabili matatizo na kupata manufaa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika. Ili kufikia lengo la kukidhi mahitaji ya kiuchumi na kijamii ya Wanachama.

 1. Madhumuni ya Chama

  Madhumuni ya kuinua na kustawisha hali ya uchumi na maisha yao kwa kuanzisha na kumiliki TANESCO SACCOS kidemokrasia, kuchangia mtaji na kukubali kuyakabili matatizo na kupata manufaa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika.

 2. Dira ya Chama

  Kuwa saccos ya mfano inayotoa huduma bora za ukusanyaji wa akiba na utoaji wa mikopo nafuu.

 3. Maono ya Chama

  Kuboresha hali za uchumi na kijamii za wanachama kupitia mikopo nafuu.

 4. Historia Fupi ya Chama

  Chama kilianza mwaka 1968 na hadi mwaka 2004 kilikua na wanachama 315 na jumla ya akiba za wanachama zipatazo Tsh. milioni 533. Mwaka 2004 yalifanyika mageuzi makubwa ya uongozi ili kukiboresha chama, na mafanikio yake yalikua makubwa kwani chama kiliweza kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia wanachama 2906 na akiba kufikia takribani bilioni 6 Julai 2009. Mapato ya kila mwezi yameongezeka kutoka millioni 25 mwaka 2004 na hadi kufikia milioni 630, Mei 2010.

Wadau Wetu