Bodi ya Chama inawatangazia wanachama wote wawakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama, kwamba Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 utafanyika mjini Morogoro tarehe 04 Oktoba 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Cate, uliopo mkoa wa Morogoro kuanzia saa 02.00 asubuhi.
AJENDA:
- Kufungua Mkutano
- Muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2024
- Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa mwaka 2024
- Taarifa ya Bodi ya Chama
- Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2024
- Taarifa ya Kamati ya Usimamizi
- Mpango kazi na Bajeti ya mwaka 2026
- Kuidhinisha Wakaguzi wa hesabu za mwaka 2025
9. Kuidhinisha ukomo wa Madeni
- Pendekezo la Honoraria kwa Viongozi 2024
- Mengineyo
- Kufunga Mkutano
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
- Mengineyo yatumwe Makao Makuu ya Chama kabla ya tarehe 09.2025
- Wawakilishi watajisajili katika Ukumbi wa Hotel ya Cate siku moja kabla ya Mkutano (03.10.2025)
- Wawakilishi wote wanatakiwa kuja na vitambulisho vyao vya
- Nakala chepe ya kabrasha la Mkutano Mkuu litatumwa Matawini kwa njia ya mtandao tarehe 26.09.2025. Nakala halisi na taarifa mbalimbali za Mkutano zitatolewa katika viunga vya Ukumbi wa hoteli ya Cate.