MIKUTANO YA DONDOO NA TAARIFA KWA WANACHAMA MATAWINI

 

Chama kinawatangazia Wanachama wote kuwa, kinatarajia kuanza kufanya Mikutano ya Dondoo za Mkutano Mkuu wa mwaka 2024 katika matawi yake nchi nzima kuanzia tarehe 07.09.2024 kutekeleza dhana ya ushirikishwaji wa wanachama katika mipango ya Chama.

Agenda za Mkutano:

  • Maboresho katika Sera ya Mikopo
  • Elimu ya Fedha :
  • Usimamizi wa Fedha Binafsi
  • Bajeti na Vipaumbele kulingana na Umri
  • Dondoo
  • Taarifa: Ugawaji wa Kadi za FOSA zilizokwisha muda (Expired)
  • Uchaguzi Mdogo (kwa nafasi za uwakilishi zilizo wazi)

 

TANBIHI:

  1. Ofisa wa Chama atakuwepo siku moja kabla ya siku ya Mkutano kwa ajili ya kuendesha clinic ya huduma za Chama, na kutatua changamoto za wanachama.
  2. Wanachama wote mtatakiwa kuwa na kitambulisho halali wakati wa Usajili siku ya kikao.
  3. Rejesta ya maudhurio itafungwa dakika 45 baada ya Mkutano kuanza.
  4. Chama kinawakaribisha wafanyakazi wote wa Shirika wasio wanachama kuja na kupata elimu kuhusu bidhaa za Chama na kuwasajiliwa.
  5. Fedha za maandalizi zitatumwa kwa Mwenyekiti/Katibu wa tawi.

 

Download

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *